Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 25, 2016

YANGA YASEMA ENDAPO TFF ITAKUBALI KULETA WAAMUZI WA NJE HAINA TABUUONGOZI wa Yanga umekubali kuchezeshwa na waamuzi kutoka nje ya nchi kwenye mechi yao na   Simba endapo Shirikisho la Soka nchini (TFF) litakubali.
Hivi karibuni Msemaji wa Simba, Haji Manara aliweka wazi kuwa hawataingiza timu uwanjani dhidi ya Yanga endapo mchezo huo utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini kwa madai kuwa hawatendewi haki.
Hata hivyo jana TFF, kupitia kwa Ofisa habari wake, Alfred Lucas, lilisema kanuni za ligi hazijakataza waamuzi kutoka nje ya Tanzania bali suala hilo linahitaji mjadala wa kina baina ya pande zote.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, amesema kuwa kama TFF itakubali ombi la Simba mechi yao kuchezeshwa na waamuzi kutoka nje ya Tanzania hawatakuwa na pingamizi ila ametoa angalizo kuwa tukio hilo litashusha hadhi ya waamuzi nchini.
"TFF wakikubali tukicheza na Simba mchezo uchezeshwe na waamuzi kutoka nje hatuna shida ila wanatakiwa kulitazama kwa umakini suala hili kwakuwa linaweza kuleta mpasuko kwenye soka letu," alisema Sanga.

Sanga alisema waamuzi wanafanya kazi kubwa za kutafsiri sheria 17 za soka na pia sio kazi rahisi kama watu wanavyochukulia hivyo TFF inatakiwa kufanya maamuzi sahihi kwa mustakabali wa soka letu na waamuzi.
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuingia kambini Jumatatu tayari kwa maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi.