Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, November 25, 2016

JKT QUEENS NI MWENDO WA GWARIDE KWA KILA TIMUTIMU ya Soka ya wanawake, JKT Queens imefunga timu ya Viva ya Mtwara mabao 12-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam jana.
Mchezo huo ambao ulikuwa wa upande mmoja ulihudia JKT Queens wakienda mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 4-0 na kipindi cha pili walifunga mabao nane mengine.
Shujaa wa mchezo huo alikuwani mshambuliaji wa JKT Queens, Asha Rashid 'Mwalala' ambaye alifunga mabao sita akifuatiwa na Donesia Anthony ambaye alifunga mabao matano na Johari Hamis ambaye alihitimisha karamu kwa kufunga bao moja.
Dakika ya 80 Kipa wa Viva, Zuhura Abdallah aliumia baada ya kugongana na nahodha wa JKT Queens wakati akiwa kwenye harakati za kuokoa mpira kwenye eneo lake na kulamika kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya Amana kwa uchunguzi zaidi.
 Zuhura alipigwa teke la tumboni hali iliyomsababishia maumivu makali na kushindwa kuendelea na mchezo na nafasi yake kuchukuliwa na Husna Kombo.
Akizungumza baada ya mchezo, kocha wa JKT Queens, Robert Ngoliga alisema dhamira yao ni kuchukua ubingwa na ndio maana wachezaji wake wanajitahidi kuufunga mabao mengi iwezekanavyo.
"Dhamira yetu ni ubingwa na ndio maana tumefanya usajili wa uhakika na kila mechi tunahesabu kama ni fainali kwetu," alisema Ngoliga.
Kwenye mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa Samora Iringa, Panama iliifunga Baobab bao 1-0.