Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, November 16, 2016

MEYA SEONGNAM KUSAPOTI TFF

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi jana alimtembelea Mstahiki Meya wa Jiji la Seongnam, Jae-myung Lee kumshukuru kwa namna ambavyo ameipokea timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys.
Serengeti Boys walioko Korea kwa michezo ya kirafiki ya kimataifa ambako Jiji la Seongnam ni mshirika wa klabu ya Seongnam FC ambao ndio wenyeji wa timu yetu ya vijana ambayo ilifanya michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa.

Katika mazungumzo kocha huyo, Meya Jae-myung Lee aliiakikishia TFF kuwa jiji lake litaendelea kushirikiana na shirikisho katika kuendeleza mpira wa vijana wakike na wakiume.

Katika kumtembelea Meya huyo, Rais Malinzi aliambatana na Mkurugenzi wa Ufundi, Salum Madadi na benchi nzima la ufundi, linaloongozwa na Kocha Bakari Nyundo Shime na msaidizi wake, Muharami Mohammed Sultan pamoja na Mshauri Mkuu wa Maendeleo ya soka la vijana, Kim Poulsen.

Baadaye jioni ya Novemba 15, 2016 Rais Malinzi alikutana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Korea Kusini (KFA), Chung Mong-Gyu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Hyundai.

Rais wa KFA Mong-Gyu naye alihakikishia TFF kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Korea litasaidia kuendeleza soka la vijana Tanzania sambamba na kusaidia mafunzo ya makocha..

No comments:

Post a Comment