Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 22, 2016

SERENGETI BOYS KUCHEZA NA CONGO BRAZAVILLE SEPTEMBA 5.



 IMG-20160821-WA0013
TIMU ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Serengeti Boys sasa itakutana na Congo Brazaville baada ya kuitoa Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-1
Jana kwenye Uwanja wa Chamazi vijana wa Serengeti boys waliwapa furaha watanzania baada ya kuifunga Afrika Kusini mabao 2-0  na kukata tiketi ya kusonga mbele kwenye hatua ya kufuzu fainali za Afrika kwa vijana zitakazofanyika Madagascar mwakani.
Katika mchezo wa awali timu hizo zilitoka sare ya kufungana mabao 1-1 wiki mbili zilizopita nchini Afrika Kusini.

Serengeti walionesha kandanda safi kipindi cha kwanza na kuwaacha Amajimbos wakiwa hawaamini kilichokuwa kikitokea katika mtanange huo lakini baada ya mchezaji wao kutolewa kwa kadi nyekundu walipunguza mashambulizi.

Dakika ya 36 Mohamed Rashidi aliipatia Serengeti bao la ufunguzi baada ya kumalizia krosi safi ya Israel Patrick upande wa kulia wa uwanja.

Mchezaji Ally Hamisi alioneshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 45 iliyopelekea kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya mchezaji wa Amajimbos.

Mshambuliaji Muhsin Makame aliipatia Serengeti bao la pili dakika ya 85 kufutia mpira wa krosi uliopigwa na Mohamed Rashidi.

Serengeti sasa itamenyana na Congo Brazaville Septemba 5 na endapo itafanikiwa kuiondoa itafuzu kwenda Madagascar.

No comments:

Post a Comment