YANGA kesho
inashuka dimbani kumaliza ungwe ya mwisho hatua ya makundi Kombe la Shirikisho
Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa ajili
ya kusaka heshima.
Mchezo huo
utachezwa saa tisa na nusu jioni kwa saa za Afrika Mashariki kwenye uwanja wa
Stade TP Mazembe.
Ni mchezo wa
kusaka heshima kwa kuwa wamekwishatolewa kwenye mashindano, timu mbili
zilizofuzu ni TP Mazembe yenye pointi 10
na Medeama ya Ghana yenye pointi nane ambazo ikiwa Yanga itashinda au kupoteza
haiendi popote na wala hatazifikia.
Katika mchezo
wa kwanza Yanga ilipoteza dhidi ya timu TP Mazembe kwenye uwanja wa Taifa,
baada ya kufungwa bao 1-0. Ni mchezo ambao Yanga itamaliza kwa heshima kama
itashinda ikiwa na pointi saba.
Ikumbukwe
mwaka 1998 Yanga ilishiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na kufikia hatua hiyo
lakini haikushinda mchezo hata mmoja.
Mwaka huu
inaonekana kuna mabadiliko baada ya kushinda angalau mchezo mmoja dhidi ya TP
Mazembe na kupoteza miwili dhidi ya Medeama na Mazembe na kupata sare moja
dhidi ya Medeama kwenye uwanja wa nyumbani, Taifa.
Timu
zilizoko kwenye kundi moja A, Medeama itachuana na Mo Bejaia nchini Algeria
kumaliza mchezo wa mwisho, lakini kama Medeama itashinda au kutoka sare
itajiongezea pointi lakini kama Mo Bejaia yenye pointi tano itashinda basi
zitalingana kwa pointi hivyo, mshindi huenda akaamuliwa kwa idadi ya magoli.
Kocha wa
Yanga Hans Pluijm alisema licha ya kutolewa hakuwezi kuwakatisha tamaa na
kushindwa kufanya vizuri katika mchezo wa mwisho.
Alisema
ushindi ni muhimu sio tu kwa timu kuweka rekodi bali hata kwa wachezaji
watakaocheza kwa juhudi ni nafasi yao kujiuza.
“Tunahitaji
kushinda mchezo huu na tunauchukulia kwa ukubwa ili tumalize salama na
kujiwekea rekodi ya kipekee,”alisema.
No comments:
Post a Comment