KIPA wa Liverpool Loris Karius amevunjika Mkono na atakuwa nje kwa Wiki 8 hadi 10.
Karius, Raia wa Germany mwenye Miaka 22, aliumia Juzi Jumatano wakati Liverpool inafungwa 1-0 na Chelsea huko Marekani na sasa atarejea Uingereza kufanyiwa Upasuaji.
Kipa huyo alijiunga na Liverpool Mwezi Mei kutoka Mainz kwa Dau la Pauni Milioni 4.7.
Habari za ndani toka Liverpool zimedai Meneja Jurgen Klopp alitaka kumfanya Karius kuwa Kipa Namba 1 na kumpiga Benchi Simon Mignolet na kuumia huku kutamfanya aikose Mechi yao ya kwanzabya Ligi Kuu England Msimu wa 2016/17 hapo Agosti 14 dhidi ya Arsenal.
Kipa mwingine wa rizevu wa Liverpool ni Mkongwe Alex Manninger mwenye Miaka 39 ambae aliwahi kuichezea Arsenal kati ya 1997 na 2002 na Mwezi uliopita kutemwa kutoka Klabu ya Germany FC Augsburg na Mwezi uliopita Liverpool kumsaini kwa Mkataba wa muda mfupi.
No comments:
Post a Comment