Wanamichezo nchini
wameaswa kutojihusisha na matumizi ya dawa au mbinu za kuongeza nguvu katika
michezo ili kuepuka na madhara yanayojitokeza ikiwemo kuzorotesha sekta ya
michezo.
Wito huo umetolewa
leo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura
alipokuwa akiwaaga wanamichezo wanaoenda kushiriki mashindano ya Olimpiki kwa
mwaka 2016 yanayofanyika Jijini Rio dejaneiro nchini Brazil.
Mhe. Anastazia
Wambura amesema kuwa wanamichezo wengi duniani kwasasa wanakabiliwa na
changamoto kubwa ya matumizi ya dawa na mbinu za kuongeza nguvu mwilini katika
michezo mbalimbali.
“Niwatake
wachezaji,madaktari na viongozi wa michezo mbalimbali kuhakikisha kuwa hakuna
mchezaji anajejihusisha na vitendo vya aibu na kwa pamoja tuungane na kupinga
jambo hili kwa kujali afya na ushindani uliopoa” alisema Mhe. Anastazia.
Aidha amewataka
viongozi wote wa michezo, waalimu na madaktari wa michezo kuungana kwa pamoja
kupiga vita matumizi ya dawa za kuongeza nguvu michezoni kwa kutoa elimu kwa
wanamichezo wao na wasisite kutoa adhabu kali pale inapothibitika mwanamichezo
amejihusisha na matumizi ya dawa hizo.
Kwa upande wake
katibu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Filbert Bayi ameahidi kutekeleza suala
hilo kwa kutoa elimu kwa waalimu na wanamchezo juu ya madhara ya matumizi ya
dawa za kuongeza nguvu za mwili katika michezo.
No comments:
Post a Comment