Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 1, 2016

AVEVA AKUBALI MO ....BAADA ya wanachama wa klabu ya Simba kupitisha kwa kauli moja mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu hiyo katika mkutano mkuu uliofanyika hii leo, Rais wake Evans Aveva amemtaka mfanyabiasha Mohamed Dewji 'MO' aandike barua rasmi ya kutaka kufanya uwekezaji.

 
 
Mkutano huo uliofanyika katika Bwalo la Maafisa wa Polisi Oysterbay ulikamilika kwa wanachama hao  kupitisha kwa kauli moja mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu hiyo kutoka mfumo wa uanachama kwenda kwenye utaratibu wa uwekezaji kwa maana ya Hisa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo Aveva alisema "Kwavile wanachama tumekubaliana kwa kauli moja kufanya mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu yetu, basi namtaka MO kama yupo tayari aandike barua rasmi ya kutaka kuwekeza."

"MO ni kijana mwenye mapenzi makubwa na Simba na Mungu amemjalia kipato kama yuko tayari ni nafasi yake sasa kuandika barua kwetu na kufuata utaratibu ambao utawekwa hadharani na kamati ya utendaji," alisema Aveva.

Mashabiki na wanachama wa timu hiyo wamefurahishwa na hatua hiyo ambayo wanaamini itawasaidia kufanya vizuri na kurejesha makali yaliyopotea kwa miaka kadhaa iliyopita.

Julai 29 MO alizungumza na vyombo vya habari kuelezea azma yake ya kutaka kufanya uwekezaji mkubwa ndani ya klabu hiyo kwa kutoa kiasi cha shilingi 20 bilioni.