Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, August 1, 2016

MO AANZA KAZI SIMBA



 

KUMEKUCHA Msimbazi, baada ya mkutano mkuu wa wanachama wa Simba kuridhia mabadiliko, mfanyabiashara aliyetangaza nia ya kuwekeza katika klabu hiyo Mohamed Dewji 'Mo' amewaita viongozi awakabidhi fungu la usajili.

"Kulikuwa na kikao kwa Mo muda mfupi uliopita,  amemwagiza mtu wake wa karibu awatafute viongozi wa Simba ili awape hela za usajili kabla dirisha halijafungwa. Na anataka waende kamati ya utendaji yote ili awakabidhi kama alivyoahidi Ijumaa," kilifafanua chanzo chetu ndani ya mchakato huo.

Pia bilionea huyo amewataka viongozi hao waende na nyaraka za maamuzi ya mkutano mkuu wa leo juu ya ofa yake aliyotoa ya kuweka kiasi cha sh 20 bilioni ili apewe hisa za 51%

No comments:

Post a Comment