Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 20, 2016

MALINZI APONGEZA UONGOZI MPYA DOREFA

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameupongeza uongozi mpya wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma ulioingia madarakani Jumamosi Julai 16, 2016.

Akizungumza na wandishi wa habari, Malinzi alisema viongozi waliofanikiwa kuingia madaraka wana kazi ya kusimamia soka na kuhakikisha kanuni na sheria za soka zinafuatwa ili kuleta maendeleo na kuondoa malumbano.

“Nawapongeza wote waliochaguliwa kuongoza DOREFA ila wajue kuwa uongozi ni dhamana hivyo wana Dodoma wanatarajia kuona soka linachezwa bila kuwa na migogoro”, alisema Malinzi

 Waliofanikiwa kuingia madarakani ni Mulamu Nghambi aliyeshinda nafasi ya Uenyekiti kwa kupata kura zote 27 wakati Makamu Mwenyekiti ni Geofrey Ngolly aliyepata kupata 25.

Katibu Mkuu ni Mussa Kissoy aliyevuna kura 19 kwa kumshinda Abubakar Ibrahim aliyepata kura nane na Katibu Msaidizi ni Abdallah Ibrahim aliyeshinda kwa kura zote 27.

Dickson Kimaro alishinda nafasi ya Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Mwakilishi wa klabu mbalimbali ikichukuliwa na Mohammed Aden na
wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Esther Ntomola, Morice Sarara na Lister Manyara  
@@@@@@@@@@@@@@@@@
Na Rahel Pallangyo

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linatarajia kutoa madawati 200 ikiwa ni sehemu ya mapato ya Ngao ya Hisani utakaochezwa Agosti 17, 2016.

Akizungumza na wandishi wa habari, Afisa habari wa TFF, Alferd Lucas, alisemna TFF inaunga mkono juhudi za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na juhudi za Serikali kwa katika kuhakikisha vijana wa Kitanzania wanakuwa na mazingira bora ya kupata elimu.

“TFF imeona umuhimu wa kusaidia elimu ya Tanzania ndio maana imeamua
kutoa sehemu ya mapato yake kama mchango wa kusaidia madawati kupitia mchezo wa ngao ya jamii utakaochezwa Agosti 17 kuashiria msimu mpya wa Ligi Kuu”, alisema Lucas.

Pia Lucas alisema  TFF inamshukuru Katibu Mkuu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah kwa juhudi za kuendelezaa mpira wa miguu na kuutumia katika kuliletea Taifa maendeleo.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania litaendelea kushirikiana na Ofisi ya Bunge Sports Club katika kufanikisha mashindano mbalimbali hasa mchezo wa Hisani kati ya Simba Sports Club na Young African (Wabunge) utakaofanyika hapo baadaye kwa mujibu wa ratiba na uratibu wa Bunge.
Mchezo wa Ngao ya Jamii utazikutanisha Yanga na Azam FC na utachezwa Agosti 17 kwenye Uwanja wa Taifa kuashiria msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

No comments:

Post a Comment