Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 20, 2016

MAKOCHA WA LESENI A WATAKIWA KWENDA KUENDELEZA SOKA

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi, amewataka makocha wanaoshiriki kozi ya ukocha wa leseni A, kwenda kutumia elimu hiyo kusaidia na kuendeleza soka.

Malinzi aliyasema hayo jana wakati akifungua kozi hiyo ambayo inashirikisha makocha 20 na kufanyika kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

“Ndugu zangu makocha nawasihi mnapohitimu kozi hii msiende kuweka vyeti vyenu ndani bali mkawe chachu ya mafanikio ya soka kwani kwa idadi ya makocha 23 ambao wana leseni A ni makocha saba tu ambao wanafundisha”, alisema Malinzi.

Pia Malinzi alisema ikimaliza kozi hii Tanzania itakuwa na makocha 43 wenye leseni A jambo ambalo ni idadi ndogo ikilinganishwa na Tanzania ambayo ina watanzania milioni 50.

Pia Malinzi alisema kuanzia msimu huu mpya wa ligi makocha watakaoruhusiwa kuwa na timu za ligi kuu ni wale wenye leseni A na kwa daraja la kwanza ni wenye leseni B huku akisema wasaidizi watatakiwa kuwa na leseni C.

Kozi hii itakuwa inafendeshwa na mkufunzi Sunday Kayuni akisaidia na Salum Madadi na itakuwa ya mwezi mmoja lakini ikimalizika wiki mbili itasimama na kuja kumalizika Novemba, 2016.

No comments:

Post a Comment