Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, July 20, 2016

SIMBA NA YANGA KUKUTANA OCTOBA MOSI


Ratiba rasmi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/2017, imetoka.
Ratiba hiyo imezingatia michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa ngazi ya klabu na timu za taifa ili kukwepa dhana yoyote ya upangaji wa matokeo na kurundikana kwa michezo.

Hii ni ratiba rasmi ukiachana na ile ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii.
Ile ya mitandao ya kijamii imekosewa anwani ya Posta ya TFF kadhalika kuonesha kuwa mchezo kati ya Azam FC na African Lyon ungefanyika Agosti 21, 2016 ilihali hii rasmi ina anwani sahihi na mchezo huo wa raundi ya kwanza ukionesha utachezwa Agosti 20, 2016.
Tunaomba familia ya soka kuegemea kwenye hii ya sasa rasmi inayotolewa na TFF. 

No comments:

Post a Comment