Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 17, 2016

MAHAKAMA YAZUILIA MALI YA NEYMAR

Mahakama moja ya Brazil imepiga tanji mali ya mchezaji nyota wa Barcelona, Neymar
Mahakama hiyo iliopo Sao Paulo ilitangaza kuwa inatoa waranti ya kuzuia mali yenye thamani ya takriban dola milioni 50 ya mchezaji huyo wa Brazil.
Mali hiyo inashirikisha ndege,jahazi la kifahari na Mali nyengine.
Neymar mwenye umri wa miaka 23 ametuhumiwa kwa kukwepa kulipa kodi kati ya mwaka 2011 na 2013 na anakabiliwa namshataka ya kujibu.
Amekana kufanya makosa yoyote.
Miongoni mwa mali zilizozuiwa ni kampuni tatu zinazomilikiwa na familia yake.
Waendesha mashtaka wanamtuhumu Neymar kwa kuanzisha kampuni ambazo zilimsaidia kulipa kiwango kidogo cha ushuru.
Wanataka alipe dola milioni 16 kama kodi ambayo haikutangazwa.
Mahakam hiyo iliagiza mali yake kupigwa tanji ili kuhakikisha kuwa anafanya malipo hayo pamoja na faini.
Hata hivyo Neymar anaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama na kwamba sio rahisi kwa yeye kuhudumia kifungo,kulingana na mkaguzi mmoja wa maswala ya fedha.