Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, February 17, 2016

RONALDO AKERWA NA MASWALI KWENYE MAHOJIANO ALIPOTAJIWA MESSI, SUAREZ, NEYMAR

CRISTIANO RONALDO alikatiza Mahojiano na Wanahabari huko Rome, Italy hapo Jana alipoulizwa kuhusu Mastraika Watatu wa Barcelona Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar.
Real Madrid wapo huko Rome kucheza Leo na AS Roma katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONS LIGI.
Akiwa pamoja na Kocha wake Zinedine Zidane, Ronaldo aliulizwa ikiwa urafiki wa karibu sana wa Messi, Suarez na Neymar ndio umewafanya wafunge Bao 22 zaidi ya Mastraika wa Real, yeye, Bale na Benzema, Msimu huu, Ronaldo alijibu: "Hilo unasema wewe. Nilipokuwa Man United na Paul Scholes, Ryan Giggs na Rio Ferdinand, tulizungumza tu 'Habari za Asubuhi' na 'Usiku Mwema' na tulitisha Uwanjani!"

"Hatukukumbatiana na kupigana mabusu. Si lazima nitoke kula Chakula cha Usiku au kuwaalika kwangu. Muhimu ni kuelewana Uwanjani. Vyakula na Mabusu na kukumbatiana havina maana yeyote."
Alipoulizwa kuhusu Messi kupiga Penati aliyompasia Suarez na kufunga Juzi Jumapili, Ronaldo alijibu: "Najua kwa nini alifanya vile na sisemi zaidi!"

Kisha akaibuka Ripota aliemtibua Ronaldo alipohoji Staa huyo kutofunga katika Mechi 4 za Ugenini na Ronaldo kujibu: "Unaweza kumtaja Mchezaji mmoja aliefunga Bao nyingi Ugenini kupita mimi tangu nitue Spain? Hapana huwezi, hakuna hata mmoja! Kwa herini wote!"
Hapo Ronaldo akatimka Ukumbini na kumwacha Kocha wake Zidane akicheka.