Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 5, 2015

RATIBA LIGI KUU ENGLAND WIKIENDI HII...JUMAMOSI NI STOKE vs MAN CITY KISHA ARSENAL vs SUNDERLAND, MAN UNITED Vs WEST HAM


Mwezi huu wa 12 mashabiki na wachambuzi walio wengi wataka kuona ni Timu gani na zipi zitakuwa juu kwenye Top 4' kwa maana timu nyingi zinapishana kwa namba ndogo sana zilizopo juu. Huku Klabu Vigogo huko England, Manchester City, Manchester United na Arsenal ambazo ziko juu kwenye Msimamo wa Ligi Kuu England, zitaingia kwenye Mechi zao za Wikiendi hii zikiwakosa Mastaa wao muhimu wengi wao wakiwa ni Majeruhi.
Man United, ambao wako Nafasi ya 3 kwenye Ligi, wataingia kwenye Mechi yao ya Nyumbani Old Trafford kucheza na West Ham bila ya Kepteni wao Wayne Rooney ambae ameumia Enka.


Maumivu hayo pia yatamfanya Rooney kuikosa Mechi muhimu ya Man United ya mwisho ya Kundi B la UEFA CHAMPIONS LIGI Jumanne ijayo huko Germany dhidi ya Wolfsburg.
Pia, Man United itamkosa Beki wao wa Argentina, Marcos Rojo, ambae aliumia Bega Mazoezini.
Majeruhi wengine wa Man United ni Phil Jones na Ander Herrera.
Man City, ambao ni Vinara wa Ligi, watazuru Britannia Stadium kucheza na Stoke City na watawakosa Yaya Touré na Sergio Agüero ambao wana maumivu.
Lakini Kipa wao, Joe Hart, baada ya kusumbuliwa na Misuli za Pajani, yuko fiti kucheza Mechi hii ya Jumamosi.
Arsenal, ambao Jumamosi wako kwao kucheza na Sunderland, watawakosa Majeruhi Santi Cazorla, Francis Coquelin na Alexis Sanchez lakini Sentahafu Laurent Koscielny na Fowadi Theo Walcott wanaweza kurudi kuikabili Sunderland.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumamosi Desemba 5

15:45 Stoke v Man City
18:00 Arsenal v Sunderland
18:00 Man United v West Ham
18:00 Southampton v Aston Villa
18:00 Swansea v Leicester
18:00 Watford v Norwich
18:00 West Brom v Tottenham
20:30 Chelsea v Bournemouth
Jumapili Desemba 6
19:00 Newcastle v Liverpool
Jumatatu Desemba 7

23:00 Everton v Crystal Palace