Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, May 22, 2015

LIVERPOOL YAFUTA MKUTANO NA RAHEEM STERLING

Sakata la Winga wa Liverpool Raheem Sterling kugomea Mkataba mpya na kung'ang''ania kuihama Klabu hiyo limefika pabaya baada ya Liverpool kufuta Mkutano uliokuwa ufanyike Ijumaa Jioni na Mchezaji huyo pamoja na Wakala wake.
Hatua hii ya Liverpool imekuja baada ya Wakala wa Sterling, Aidy Ward, kunukuliwa akisema kuwa Sterling, Fowadi wa England mwenye Miaka 20, hatasaini Mkataba mpya na Liverpool hata akipewa Mshahara wa Pauni 900,000 kwa Wiki.
Sterling, ambae Mkataba wake wa sasa na Liverpool unaomlipa Pauni 35,000 kwa Wiki unamalizika 2017, amegoma kusaini Mkataba mpya ambao ungemlipa Pauni 100,000 kwa Wiki na kudaiwa kutaka kuihama Liverpool.
Wakala wa Sterling, Aidy Ward, amekaririwa na Gazeti la Uingereza la Evening Standard kusema: "Sijali Klabu hiyo inazungumza nini. Sterling hatasaini. Hatasaini kwa Pauni Laki 7, 8, 9 kwa Wiki. Hatasaini!"
Vile vile inadaiwa, Wakala huyo aliwashutumu na kuwatukana Wachezaji wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher, John Barnes na Robbie Fowler, walioongoza kumkandiya Sterling kwa kutaka kuhama.
Hadi sasa haijulikani Sterling anataka kwenda wapi huku Man City, Arsenal, Chelsea, Real Madrid, Bayern Munich na hata Man United zikivumishwa kumsaka.

No comments:

Post a Comment