SERIKALI
kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo imeunda kamati maalumu kwa ajili
ya kuisaidia timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ili iweze kufanya vizuri
kwenye michezo yake iliyobakia ya kufuzu michuano ya Kombe la dunia 2014.
Hivi
karibuni Stars ilifanikiwa kuifunga Morocco mabao 3-1 hivyo kufanikiwa kujiweka
katika nafasi nzuri kwenye kundi C walilopo wakiwa na timu zingine za Ivory
Coast na Gambia. Msimamo wa kundi hilo mpaka sasa Stars wako katika nafasi ya
pili wakiwa na alama sita, nyuma ya vinara Ivory Coast wanaoongoza kwa alama
saba na Morocco ni ya tatu wakiwa na alama mbili wakati Gambia wao wanashikilia
mkia wakiwa na alama moja.
Kutokana na matokeo hayo wizara kupitia waziri wake
Fenela Mukangara wameipongeza timu hiyo kwa kuweka matumaini hai ya kufuzu
michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Brazil 2014. na kwa kuzingatia
hilo wizara imeamua kuunda kamati maalumu kwa ajili ya kuongeza hamasa ya
ushindi kwa Stars ili iweze kuweka historia kwa kushiriki michuano ya Brazil. Jukumu
la msingi la Kamati iliyoundwa ni kuhakikisha Taifa Stars inawezeshwa na
kuandaliwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuunda kikundi cha kuishangilia timu ya
Taifa ndani na nje ya nchi.
Wajumbe wa
Kamati ya Taifa Stars Stars itakayoongozwa na Mhe. Mohamed Dewji ni hawa
wafuatao:-
Mhe Mohamed
Dewji - Mbunge
Bi. Teddy
Mapunda - Montage
Dkt.
Ramadhani Dau - Mkurugenzi Mtendaji NSSF
Bw. Dioniz
Malinzi - Mwenyekiti BMT
Bw. Abji
Shabir - New Africa Hotel
Bw. George
Kavishe - TBL
Mhe. Mohamed
Raza - Zanzibar
Rais wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Bw. Joseph
Kusaga - Clouds
Mhe. Kapt.
John Komba - Mbunge
Mhe. Zitto
Kabwe - Mbunge
Kamati hiyo
iliyoteuliwa leo, inatakiwa kuanza kazi kazi mara moja. Hadidu za rejea
zitakazowaongoza kutekeleza majukumu yao chini ya Kamati hii watazipata kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kamati itashirikisha wadau
mbalimbali kadri itakavyoona inafaa. Serikali inaahidi kutoa ushirikiano
utakaohitajika katika kuhakikisha Kamati hii inafanya kazi vizuri ili
kuiwezesha Taifa Stars kushinda Mechi zote zilizombele yetu.
No comments:
Post a Comment