MSHAMBULIAJI Paul Kiongera jana ameingia kambini Simba SC visiwani Zanzibar na leo anatarajiwa kuanza mazoezi.
Kiongera alisajiliwa msimu uliopita, lakini akaachwa baada ya nusu msimu akiwa amecheza mechi tano na kufunga mabao mawili tu, kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti.
Mwanzoni mwa msimu huu, Simba SC ilimtoa Kiongera kwa mkopo KCB ya kwao, Kenya ili akajiimarishe zaidi kabla ya kurejea kazini Msimbazi.
Na jana mpachika mabao huyo anayesifika nchini kwao kwa ujuzi wa kufunga ameingia kambini kujiandaa kuanza kazi tena Msimbazi.
Sasa Kiongera atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaosajiliwa katika dirisha dogo Simba SC na zoezi hilo likifanikiwa ina maana atacheza mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Azam FC Desemba 12 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwa hisani ya Bin Zubery Blog
No comments:
Post a Comment