MABEKI wa Yanga,
Kelvin Yondani, Rajabu Zahir pamoja na kiungo Athumani Idd 'Chuji', wameanza
kuleta matumaini katika kikosi cha mabingwa hao watetezi, baada ya juzi kuanza
mazoezi mepesi.
Yondani aliumia
mguu katika mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Azam, Chuji aliumia goti katika
mechi ya kwanza kwenye michuano ya Ligi Kuu dhidi ya Ashanti United, huku Zahir
akiumia paja katika mazoezi.
Wachezaji hao
wanatarajiwa kujiunga na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao ya tatu ya
Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City, wakati wowote kuanzia leo, kutokana na hali zao
kuonekana kuwa zinaridhisha.
Katika mazoezi
yaliyofanyika jana kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola, wachezaji hao
walionekana kufanya mazoezi mepesi peke yao pembeni mwa uwanja huo.
Katika hatua
nyingine, Kocha msaidizi wa timu hiyo, Fredy Minziro, amesema kuwa
wana matumaini makubwa kuondoka na ushindi kwenye mechi yao inayofuata dhidi ya
Mbeya City, itakayochezwa Septemba 14 katika dimba la uwanja wa Sokoine, jijini
Mbeya.
Alisema katika
mechi hiyo, ushindi ni lazima ambapo kikosi chao kipo kamili na wanatarajia
wachezaji wote watakuwa fiti.
"Tutaendeleza
wembe ule ule katika mechi yetu ijayo na kikosi chetu kipo vizuri pamoja na
wachezaji wote waliokuwa majeruhi wanaendelea vizuri na tuna imani tutakuwa
No comments:
Post a Comment