Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, December 5, 2015

Raphael Kiongera awasili rasmi Zanzibar


Raphael Kiongera awasili rasmi Zanzibar

Katika muendelezo wa kuboresha kikosi cha Simba, mchezaji Raphael Kiongera amewasili rasmi jioni hii ya leo katika kambi ya Simba visiwani Zanzibar.
Mshambuliaji huyu wa kimataifa amewasili leo jioni visiwani Zanzibar akitokea Kenya ambapo alikuwa akiitumikia klabu ya KCB kama mchezaji aliepelekwa kwa mkopo. Akiwa katika klabu ya KCB Kiongera aliweza kupigiwa kura na wapenzi wengi wa soka nchini humo na kuweza kuwa mchezaji bora wa mwezi Agosti.
Simbasports.co.tz ilipata nafasi ya kuongea na Kiongera na kusema “nashukuru sana kwani ni furaha yangu kubwa sana kurudi tena katika klabu yangu ya Simba, ninachoweza kusema kwa sasa ni kuwa mashabiki na wapenzi wangu na hata wa soka la Tanzania kwa ujumla wategemee mambo mazuri kutoka kwangu”.
Simbasports.co.tz itaendelea kukupatia habari mbalimbali kuhusiana na kambi ya Simba iliyopo visiwani Zanzibar kadri zinavyoendelea kupatiakana.
Unataka kuwa wa kwanza kupata habari za klabu yako ya Simba tuma neno Simba kwenda namba 15460 utatumiwa ujumbe jibu “OK” nawe utakuwa umejiunga na huduma ya Simba News. Huduma itakayokuwezesha kupata habari za Simba popote ulipo kwa wateja wa Tigo na Vodacom.