Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Friday, May 22, 2015

SUNDERLAND YAIBUA VIPAJI TANZANIA, YATOA MAFUNZO SHULE BULYANHULU!


Klabu ya Ligi Kuu England Sunderland hivi karibuni imetembelea Tanzania ikiongozwa na Mkuu wao wa Kuendeleza Soka Kimataifa, Graham Robinson, ambae alizuru Migodi Miwili inayomilikiwa na Acacia Mining ili kutoa Mafunzo ya Soka kwa Jamii zinazoishi jirani na Migodi hiyo.
Acacia Mining plc, ndiyo inayomiliki Migodi ya Dhahabu ya Bulyanhulu, Buzwagi na North Mara.
Ziara hiyo ya Graham ni Mradi wa pamoja wa Klabu ya Sunderland na Acacia Mining ili kutoa Mafunzo ya Soka na Ukocha kwa Timu za Migodi hiyo na Makocha wao.

Mafunzo hayo yalifanyika Bulyanhulu Mine School yakijumuisha Makocha wa Timu ya Acacia pamoja na Makocha kutoka Vijiji jirani.
Akiongelea kuhusu Mafunzo hayo, Graham alisema: "Tulitoa mafunzo ya vitendo kadhaa na Makocha walishiriki kikamilifu na kuuliza maswali mengi."
"Soka ya Jamii ndio chanzo cha Wachezaji wengi na kupitia Washirika wetu Barani Afrika tuna Miradi ya muda mrefu na tunasifika kwa kuwekeza katika Programu za Elimu katika Jamii."
Baada ya Kipindi cha kutoa Mafunzo, Graham alishuhudia Mechi kati ya Shule ya Sekondari ya Bugarama na Shule ya Sekondari ya Bulyanhulu ambapo Msafara wa Sunderland ulitoa Mipira Miwili na Bendera.
Graham aliongeza: "Tunathamini sana kuhusu uhusiano mzuri ambao tunao na Tanzania na tunalenga kujitwika kwenye Jamii ambazo tunafanya nazo kazi ili kufikisha malengo huku tukiboresha maisha ya Watu."
Katika sehemu ya Ziara yake ya Tanzania, Graham pia alikutana na Maafisa wa Symbion Power na kutembelea eneo ambalo litajengwa Kituo cha Vijana cha Rais Jakaya M. Kikwete (Jakaya M. Kikwete Youth Park) pale Kidongo Chekundu Jijini Dar es Salaam.
Kituo hicho kinagharamiwa na Symbion Power na Klabu ya Sunderland inatoa msaada wa Kiufundi na wa Vitendo.

No comments:

Post a Comment