Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, August 12, 2015

JOSE MOURINHO AMKATAA DOKTA WA CHELSEA EVA CARNEIRO.

BAADA ya kumlaumu sana Dokta wa Timu ya Chelsea, Eva Carneiro, mara baada ya Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England Jumamosi iliyopita Uwanjani Stamford Bridge waliyotoka 2-2 na Swansea City, Meneja Jose Mourinho sasa ameamua Dokta huyo hatakaa tena na Benchi la Timu hiyo.
Inaaminika Mwanamama Eva Carneiro atabakia Daktari wa Timu ya Kwanza ya Chelsea lakini hataandamana na Timu kwenye Mechi wala kuhudhuria Mazoezi na hivyo Jumapili ijayo hatatarajiwa kuwepo kwenye Benchi la Chelsea wakicheza huko Etihad na Manchester City kama ilivyo kawaida yake.
Jumamosi iliyopita, Uwanjani Stamford Bridge, katika Dakika za Majeruhi huku Gemu na Swansea ikiwa 2-2 na Chelsea kuwa Mtu 10 baada ya Kipa wao Thibaut Courtois kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu, Fowadi wa Chelsea Eden Hazard alianguka chini kwa maumivu na Refa kuashiria Benchi la Chelsea na ndipo Dokta Eva Carneiro akachomoka mbio kuingia Uwanjani kama kawaida yake kwenda kutoa huduma.
Kitendo hicho kilimkera mno Mourinho na waziwazi alinaswa akimbatukia Dokta Eva Carneiro ambae nae alijibu mapigo.
Ghadhabu za Mourinho zilitokana na Chelsea kubaki na wachezaji tisauwanjani kwa dakika kadhaa kwani kisheria mchezaji akiumia ulazimika madaktari kuingia kumtibu basi anapaswa kutoka nje ya uwanjani na mchezo kuendelea na baadae refa kumruhusu arudi tena uwanjani.
Mourinho alidai Eva Carneiro hajui kusoma Mchezo.
Lakini, katika kile kinachodaiwa kumkandya Mourinho hadharani, Dokta Eva Carneiro aliposti kwenye kurasa yake ya facebook maneno haya: “Napenda kuwashukuru Watu wote kwa sapoti yao. Natoa shukrani kubwa.”

Dokta Eva Carneiro, ambae alizaliwa Septemba 15 Mwaka 1973 huko Gibraltar na ambae Baba yake ni Mhispania na Mama Mwingereza, aliteuliwa kuwa Dokta wa Timu ya Kwanza ya Chelsea Mwaka 2011 na aliekuwa Meneja wa wakati huo Andre Villas-Boas.

No comments:

Post a Comment