Vodacom na
TFF zasaini mkataba wa udhamini wa ligi kuu kwa miaka mitatu.
Dar es
Salaam, 12 August 2015; Shirikisho
la mpira wa miguu Tanzania (TFF) leo limeingia katika mkataba wa udhamini
na mdhamini Mkuu wa ligi hiyo Vodacom Tanzania, wakati maandalizi ya ligi kuu
yakiendelea.
Kampuni ya
Vodacom Tanzania inayoongoza hapa nchini kwa huduma za mawasiliano imekuwa
mdhamini wa ligi kuu kwa miaka minane iliyopita, na sasa imeingia mkataba mpya
wa udhamini kwa miaka mitatu na TFF, mkataba utakao liwezesha shirikisho hilo
kupokea fedha za udhamini kwa miaka mitatu.
Ligi kuu ya
Vodacom 2015/16 inayotarajiwa kaunza katika siku za karibuni itachezwa
katika viwanja mbalimbali na kushirikisha timu 16, zikiwemo timu za Mwadui na
Africa Sports ambazo zimepanda daraja msimu huu.
Mkuu wa
Mawasiliano na Masoko wa kampuni hiyo Kelvin Twissa, amesema kuwa kampuni ya
Vodacom iko katika mstari wa mbele katika kuunga mkono maendeleo na shughuli
mbalimbali za kimichezo ndani ya nchi.
“Wanamichezo
wote ni mabalozi wazuri katika nchi. Ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa tunawaunga
mkono katika kutambua na kukuza vipaji vyao kadri tutakavyo weza,” alisema
Twissa na kuongeza kuwa, “Kama jina linavyojulikana ligi kuu ya Vodacom,
ligi hii ni maarufu nchini na nje ya nchi na inafuatiliwa na
mamilioni ya washabiki wa soka nchini .”
Twissa amejivunia kampuni hiyo kuwa
wadhamini wa ligi kuu kwa kipindi kingine, na kufafanua kuwa mpira wa miguu
ndio unaongoza kitaifa na unapendwa na Watanzania wengi.
Mkataba huu
umehusisha pande zote ambazo ni kampuni ya Vodacom Tanzania, Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kamati ya ligi.
Kwa upande
wake Rais wa TFF, Jamali Malinzi, ameipongeza kampuni ya Vodacom Tanzania
akisema kuwa anaamini kuwa maendeleo ya sasa yatalenga zaidi katika kuunga
mkono vipaji vipya na vilivyopo ndani ya nchi.
“Kwa niaba
ya TFF, napenda kuwashukuru Vodacom Tanzania kwa kuonyesha nia na kuendelea
kuunga mkono mpira wa miguu nchini. Nasi tunaahidi kuendelea kuthamini vipaji
vya wachezaji wetu na kuhakikisha tunapata mafanikio zaidi,” alisema Malinzi.
No comments:
Post a Comment