Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, June 2, 2013

ITV KUONYESHA TUZO ZA KILIMANJARO MUSIC AWARDS LIVE

Meneja wa bia ya Kilimanjaro, George Kavishe akiongea na waandishi wa habari leo

KITUO cha Televisheni cha  ITV kimepewa tenda ya kuonyesha moja kwa moja onyesho la tuzo za muziki Tanzania, Kili Music Award itakalofanyika Juni 8,  mwaka huu kwenye ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo katika ukumbi wa Roots, Masaki, Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe amesema kwamba sababu za kuichagua ITV ni kuamini wanaweza kufanya kazi hiyo kwa ufanisi kulingana na makubaliano yao.

Pamoja na kurushwa live kupitia ITV, Kavishe amesema kwamba onyesho hilo litaonyeshwa live katika sehemu tatu tofauti nchini, ambazo wameziteua ni Mwanza eneo la Mabatini, Temeke Uwanja wa Taifa na Kilimanjaro, CCM Mkoa.

Kavishe alisema zoezi la kupigia kura wasanii kuelekea tuzo hizo zinazokwenda na kaulimbiu ya Kikwetukwetu mwaka huu lilifungwa Mei 31, mwaka huu.
Pia Kavishe alisema wasanii wa sasa wataimba nyimbo za wasanii wa zamani na wasanii wa zamani wataimba nyimbo za wasanii wa sasa.


“Kutakuwa na kitu tofauti kwa upande wa burudani, ambacho kitapendeza na kuvutia, kwa ujumla maandalizi yako vizuri na tunatarajia mambo mazuri siku hiyo,”alisema Kavishe.    

No comments:

Post a Comment