TIMU ya
Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni imefungwa mabao 6-2 na Misri kwenye
mchezo wa kutafuta kufuzu fainali za Afrika uliochezwa kwenye ufukwe wa Escape
One, Dar es Salaam jana.
Tanzania
iliuanza mchezo huo kipindi cha kwanza kwa kuifunga Misri mabao 2-1 yaliyofungwa
na Ally Rabbi na Mwalimu Akida.
Kipindi cha
pili, Misri walicharukana kuifunga Tanzania mabao matatu na kufikisha mabao 4-2
na kipindi cha mwisho wakifunga mabao mengine mawili na kufikisha mabao 6-2.
Wafungaji wa
Misri ni Yehia Ally aliyefunga manne, Islam Ahmed na Mohamed Faway waliofunga
bao moja kila mmoja.
Akizungumzia
mchezo huo, Kocha wa Stars, John Mwansasu alisema wachezaji wake walifungwa kwa
vile hawakupata muda wa kupasha mwili kutokana na kuchelewa kufika uwanjani
kutokana na foleni kwani hawakuwa na polisi wa kuwasindikiza uwanjani kutoka kambini
Bamba Beach, Kigamboni.
Pia alisema
Misri wana uzoefu na wana uwezo wa kumiliki mpira kuliko wao ila anajiandaa kwa
ajili ya mchezo wa marudiano utakaochezwa nchini Misri baada ya wiki moja
No comments:
Post a Comment