Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, February 22, 2015

TANZANIA KUKUTANA NA MISRI BAADA YA KUIFUNGA KENYA MABAO 12-9.



 
Mwalimu Akida (kulia) na Rolland Revocutus (katikati) wakimpongeza nahodha wao Ally Rabbi baada ya kufunga mabao matano peke yake kwenye mchezo huo wa jana

Ally Rabbi akipongezwa











Kikosi cha Tanzania

Kikosi cha Kenya

Wachezaji wa akiba wa Tanzania wakifuatilia mpambano

Wachezaji wa Kenya na viongozi wao wakiwa hawaamini kuwa safari yao ya kwenda Shelisheli imeishia ufukwe wa Escape one jijini Dar es Salaam

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, John Mwansasu amekiri mchezo wa raundi ya pili wa kutafuta kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Misri utakuwa na ushindani sana.

Mwansasu aliyasema hayo baada ya kufanikiwa kuondoa Kenya kwenye mchezo wa raundi ya kwanza uliochezwa ufukwe wa Escape One jijini Dar es Salaam juzi na kuifunga mabao 7-6.

Tanzania kwenye mchezo wa awali uliochezwa Mombasa nchini Kenya Tanzania ilishinda mabao 5-3 hivyo imefuzu raundi ya pili kwa kuifunga Kenya jumla ya mabao 12-9 itakutana na timu ya Taifa ya Misri kati ya Machi 7, 8 na kurudiana kati ya Machi 13, 14, 2015

“Namshukuru Mungu tumeshinda mchezo wa leo lakini bado tuna safari ndefu kwani Misri ambao ndo tutacheza nao raundi ya pili ni timu nzuri hivyo tunahitaji maandalizi mazuri na sapoti ya mashabiki”, alisema Mwansasu

Mabao ya Tanzania yalifungwa na nahodha, Ally Rabbi aliyefunga mabao matano, Kashiru Salum na Samweli John ambao kila mmoja alifunga bao moja.

Endapo Tanzania itafanikiwa kuiondoa Misri itakuwa imefuzu moja kwa moja katika fainali za Mataifa ya Afrika yatakayofanyika kwenye Visiwa vya Shelisheli April mwaka huu

No comments:

Post a Comment