MCHEZAJI wa zamani wa Simba SC,
Christopher Alex, amefariki Dunia mkoani Dodoma, baada ya kuugua kwa muda
mrefu.
Mchezaji huyo anayekumbukwa kutokana na uwezo
wake uwanjani, amefariki ikiwa ni baada ya kuteseka kwa muda mrefu.
Mapema mwaka huu Alex alisikika
katika kituo cha redio cha Uhuru FM, akilalamika jinsi viongozi wa soka wa
Simba walivyoweza kumtupa kiasi cha kushindwa hata kumjulia hali, licha ya
kuichezea timu hiyo kwa moyo wote.
Katika malalamiko yake hayo,
alitumia muda mwingi kumuomba pia nahodha wake wa zamani, Selemani Matola,
akiamini kuwa alikuwa na uwezo wa kufuatilia suala hilo kwa viongozi wake hao
wa zamani wa klabu ya Simba.
Alex ni moja ya wachezaji mahiri wa
klabu ya Simba walioitumikia klabu hiyo kwa moyo na mafanikio makubwa. Akiwa
uwanjani mwaka 2002, Alex na wenzake walifanikiwa kufuzu robo fainali ya Ligi
ya Mabingwa Afrika kwa kuwaondosha vigogo wa Afrika, timu ya Zamalek na kuzua
shangwe Tanzania na kwa nchi zote za Afrika Mashariki na Kati.
No comments:
Post a Comment