Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Sunday, February 22, 2015

MEZ B KUZIKWA KESHO



MWANAMUZIKI Moses Bushagama maarufu kama Mez B aliyefariki dunia Ijumaa iliyopita wakati akikimbizwa hospitalini atazikwa kesho katika Makaburi ya Wahanga wa Treni yaliyopo Mailimbili  mjini Dodoma.
Taarifa iliyotolewa na mama yake  Mez B, Merry Katambi alisema  shughuli ya kumuaga mwanae itafanyika Viwanja vya Nyerere Sguare Mjini hapa.
Mazishi hayo kwenye viwanja vya Nyerere yataambatana na ibada ya kumuombea na yanatarajiwa kuanza saa saba mchana.
 ‘’Mwanangu tutamzika Jumatatu (leo) katika Makaburi ya wahanga wa Treni Mailimbili ila ibada pamoja na kuuga mwili wa marehemu zitafanyika katika viwanja vya Mwalimu Nyerere’’ 
Mez B alikuwa ni mwanzilishi wa kundi la Chemba Squard ambapo alikuwa pamoja na Dar Master, Noorah na Albert Mangwea huku akitamba na nyimbo za Kikuku cha Mama Rhoda na Nimekubali.

No comments:

Post a Comment