Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 5, 2016

SIMBA, YANGA NA AZAM KIBARUANI KESHOSIMBA, Yanga na Azam FC kesho zitashuka dimbani kwenye viwanja tofauti kusaka pointi tatu ambazo zitaendelea kuwapa nafasi ya kuendelea kuingia katika vita ya ubingwa, kila mmoja akionyesha shauku na umuhimu wa kushinda ugenini.
Wekundu hao watakuwa kwenye uwanja wa Uhuru dhidi ya African Lyon, ikijivunia kushika usukani wa ligi kwa pointi 35 na kuziacha Yanga na Azam kwa tofauti ya pointi nane hadi 13.
Simba haijapoteza mchezo hata mmoja katika 13 iliyocheza, ikishinda 11 na kupata sare mbili. Mbali na rekodi hiyo bora, pia, ndio timu yenye mchezaji anaongoza kwa ufungaji Shiza Kichuya akiwa na magoli tisa.
Timu hiyo ina nafasi kubwa ya kushinda mchezo wa leo baada ya kutoka kushinda dhidi ya Stand United bao 1-0, uliochezwa Shinyanga hivi karibuni.
 Inacheza na African Lyon ambayo licha ya kutokuwa katika nafasi nzuri bado haipaswi kudharauliwa kwa kuwa haitabiriki.  Timu hiyo ina pointi 14 katika michezo 14 iliyocheza ikishika nafasi ya 11.
Yanga itakuwa kwenye uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya. Ni timu inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 27 katika michezo 13 iliyocheza. Mchezo wa leo una umuhimu mkubwa kwao kushinda kama inataka kukimbizana na Simba katika mbio za ubingwa.
Mchezo huo hautakuwa rahisi kwa kila timu, kwani zote zimetoka kupoteza michezo yao, Yanga ikitoka kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City na Tanzania Prisons ikifungwa na Ndanda FC bao 1-0.
Kuanzia msimu wa 2013 hadi sasa, Yanga imekuwa na rekodi nzuri ya kufunga au kutoka sare dhidi ya Prisons, lakini Februari mwaka huu kwenye uwanja wa Sokoine, timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.
Aidha, Azam FC itakuwa kwenye uwanja wa CCM, Kirumba Mwanza ikichuana na Mbao FC. Timu hii imeanza kurudi taratibu baada ya kushinda michezo miwili iliyopita ya ugenini. Iliifunga 1-0 Toto Africans na 3-2 Kagera Sugar.
Katika michezo 13 iliyocheza imeshinda sita, sare nne na kufungwa mitatu ikishika nafasi ya 13 kwa pointi 22. Inakutana na Mbao FC ambayo imekuwa ikizikazia timu kubwa licha ya kufungwa.
Mbao licha ya kutokuwa na uzoefu wa kutosha wa ligi, inapokutana na timu kubwa hucheza mchezo mzuri wa kujihami na kushambulia mara chache na mara unapoidharau ni rahisi kuabisha kwani ina wachezaji wanaojituma.
Timu hii bado haiko katika nafasi nzuri baada ya kupoteza michezo kadhaa iliyopita ikiwa ugenini. Inashika nafasi ya tatu kutoka mwisho, ikiwa na pointi 12 katika michezo 14.
Ndanda FC inayoshika nafasi ya 10 kwa pointi 16  itaikaribisha Stand United. Huu utakuwa mchezo mgumu kwa kila timu kwani timu hiyo ya Mtwara ni mara chache imefungwa kwenye uwanja wake msimu huu.
Pia,  Stand ni timu ambayo imekuja kivingine, iko vizuri na kwa sasa inashika nafasi ya nne, ikiwa na pointi 22 katika michezo 14 iliyocheza. Ni mchezo ambao iwapo Stand itakubali kichapo itashuka na zile zilizoko chini yake kama zikishinda zina uwezekano wa kupanda, hivyo utakuwa mgumu.
Kagera Sugar itakutana na Ruvu Shooting huko Kaitaba. Kagera inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 21 na Ruvu nafasi ya saba kwa pointi 19. Kila mmoja anahitaji ushindi kujisogeza kutoka safasi moja hadi nyingine.
JKT Ruvu itaikaribisha Toto Africans. Timu zote mbili zinafuatana kwa kushika mkia wakitofautiana kwa pointi moja. JKT ina pointi 12 na Toto 11 wote wakiwa wameshacheza michezo 14. Hii ni mechi inayohitaji ushindi kwa kila mmoja kujiondoa katika nafasi walizopo.