Kikosi cha wachezaji 18 na viongozi 11 wa timu ya
Taifa ya Benin, kimetua jijini Dar es Salaam tayari kwa mechi ya Kalenda ya
FIFA dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumapili (Oktoba 12 mwaka huu) Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam.
Wachezaji wa timu ya Benin ambayo imefikia hoteli
ya JB Belmont waliwasili jana (Oktoba 9 mwaka huu) Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere (JNIA) kwa nyakati tofauti.
Kikosi hicho kitafanya mazoezi yake ya kwanza leo
(Oktoba 10 mwaka huu) saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Gymkhana. Benin watafanya
mazoezi yao ya mwisho kesho (Oktoba 11 mwaka huu) saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.
Wachezaji walioko kwenye kikosi cha Benin ni Stephane
Sessegnon (West Bromwich Albion, Uingereza), Didier Sossa (USS Krake, Benin),
Abdel Fadel Suanon (Etoile Sportive du Sahel, Tunisia), Jodel Dossou (Red Bull
Salzburg, Austria), Sessi D’almeida (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa), Mohamed
Aoudou (JS Saoura, Algeria) na Saturnin Allagbe (Niort, Ufaransa).
Steve Mounie (Montpellier, Ufaransa), Farnolle
Fabien (Clermont Foot Auvergne 63, Ufaransa), Jordan Adeoti (Caen, Ufaransa), Michael
Pote (Omonia Nikosia, Cyprus), David Djigla (FC Girondis Bordeaux, Ufaransa) na
Seidou Baraze (Kawkab Marrakech, Morocco).
Jean Ogouchi, Centre Mberie Sportif Club, Gabon),
Nafiou Badarou (ASO Chlef, Algeria), Eric Tossavi (Avrankou Omnisport, Benin),
Fortune Ore (USS Krake, Benin) na Seibou Mama (Aspac, Benin).
Nayo Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro
Premium Lager leo (Oktoba 10 mwaka huu) itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam saa 10 jioni.
Wakati huo huo, makocha wa Taifa Stars, Mart
Nooij na wa Benin Didier Nicolle Olle watakuwa na mkutano na waandishi wa
habari kesho (Oktoba 11 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye
ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika Jengo la PPF Tower
No comments:
Post a Comment