Diego
Costa ameonyesha kutosumbuliwa na tatizo lolote la maumivu ya misuli
ya paja baada ya kuanza mazoezi na timu ya Hispania kwa mafanikio ya
kujiandaa na michezo ya kufuzu kwa Euro 2016 dhidi ya Slovakia na
Luxembourg.
Msambuliaji
huyo wa Chelsea amejiunga na mchezaji mwenzake Cesi Fabregas
wanaotoka klabu moja, pamoja na nyota wengine wanoacheza ligi soka
England akiwemo David Silva na golikipa David de Gea wa Manchester.
Timu
hiyo inayofundishwa na kocha mkongwe Vicente del Bosque, iliitandika
Macedonia goli 5-1 katika mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo, na
sasa ni zamu ya Slovakia pamoja na Luxembourg.
Costa,
amefunga magoli tisa katika mechi saba za ligi kuu soka England,
akichezea klabu yake ya Chelsea msimu huu, lakini amekuwa na wakati
mgumu kupachika magoli akiwa na kikosi cha Hispania katika michezo ya
kimataifa hivyo ni wakati mwingine wa mchezaji huyo kuonyesha makali
yake katika michezo hiyo miwili ya juma hili.
Wakati
huo huo Kocha Del Bosque, amesema kuwa hashangazwi na timu yake
kushindwa kuonyesha kiwango cha hali ya juu katika michuano ya kombe
la dunia huko Brazil, na kuongeza kuwa timu hiyo iko katika kipindi
cha mpito licha ya kupoteza muelekeo katika michuano hiyo mikubwa.
Hata
hivyo amewataka wachezaji wake kusahau yaliyopita huko Brazil, kwani
hivi sasa ana damu mpya ambazo zina ari ya kutaka kufanya makubwa, ni
bora wakawaza mwanzo mpya.
No comments:
Post a Comment