Michuano ya Ligi Daraja la Kwanza
(FDL) msimu wa 2014/2015 inaanza kutimua vumbi leo
katika viwanja tisa tofauti kwenye miji ya Moshi, Arusha, Musoma, Mwanza,
Geita, Mbozi, Songea, Mufindi na Dar es Salaam.
Kundi A litakuwa na mechi kati ya
Kimondo FC na Villa Squad itachezwa Uwanja wa Vwawa mjini Mbozi wakati Majimaji
itaumana na Ashanti United (Uwanja wa Majimaji, Songea).
Nyingine ni Kurugenzi Mafinga na
Tessema FC kwenye Uwanja wa Mufindi huku Friends Rangers ikioneshana kazi na
Lipuli ya Iringa kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam.
Kundi B ni Panone itaikabili Kanembwa
JKT (Uwanja wa Ushirika, Moshi), Oljoro JKT itapambana na Polisi Dodoma (Uwanja
wa Sheikh Kaluta Amri Abedi, Arusha), Polisi Mara na Rhino Rangers (Uwanja wa Kumbukumbu
ya Karume, Musoma).
Mechi nyingine ni kati ya Toto
Africans na Mwadui itakayofanyika Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza na Geita
Gold na Burkina Faso (Uwanja wa Waja, Geita).
No comments:
Post a Comment