Nahodha
wa Manchester United na England Wayne Rooney amesema kwa sasa ni mtu
mzima, lakini amekuwa akitafakari ni namna gani ataweza kuzuia hasira
zake mchezoni.
Rooney,
mwenye umri 28, amekosolewa vikali baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu
katika mchezo wa ligi kuu soka England ambapo United iliibuka na
ushindi wa bao 2-1 dhid ya West Ham uwanjani Old Trafford mwezi
uliopita.
Rooney
amesisitiza kuwa hivi sasa amebadilika tofauti na Yule wa zamani
ambaye alikuwa na tabia ya kukasirika kila mara, hivyo amewataka
radhi mashabiki wa united na kuongeza kuwa rafu aliyomchezea Stewart
Downing haikuwa ya kiungwana.
No comments:
Post a Comment