Waamuzi
wanaotarajia kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) msimu huu watafanya mtihani wa utimamu wa mwili (physical fitness
test) mwezi ujao.
Mtihani
huo utahusisha waamuzi wa daraja la kwanza (class one) wakiwemo pia wale wenye
beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Mbali
ya mtihani huo unaotarajiwa kufanyika kabla ya Septemba 10 mwaka huu, pia
kutakuwa na semina kwa makamishna ambao watasimamia mechi za VPL na FDL.
Hivyo
waamuzi wote wanatakiwa kutumia muda uliobaki kufanya maandalizi kwa ajili ya
mtihani huo.
No comments:
Post a Comment