Makocha
wa kombaini za mikoa zitakazoshiriki Copa Coca-Cola mwaka 2014 pamoja na
waamuzi vijana wa michuano hiyo watashiriki kozi ya ukocha na uamuzi itakayofanyika
jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu.
Kozi
hiyo itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Agosti 25 hadi 29 mwaka huu ikiwa
ni sehemu ya maandalizi michuano ya Copa Coca-Cola ngazi ya Taifa itakayochezwa
Septemba mwaka huu.
Makocha
watakaoshiriki kozi hiyo na mikoa yao kwenye mabano ni Ahmed Simba (Mwanza), Ally
Kagire (Kagera), Aloyce Mayombo (Pwani), Andrew Zoma (Tabora), Anthony Mwamlima
(Mbeya), Athuman Kairo (Morogoro), Bakari Ali (Kaskazini Pemba) na Charles
Mayaya (Shinyanga).
Fidelis
Kalinga (Iringa), Gabriel Gunda (Singida), Hafidh Muhidin Mcha (Kusini Pemba), Hamis
Mabo (Kigoma), John William (Geita), Joseph Assey (Shinyanga), Joseph Haley
(Manyara), Jumanne Ntambi (Kilimanjaro), Leonard Jima (Ruvuma), Madenge Omari (Mara),
Mohamed Muya (Dodoma), Nicholas Kiondo (Ilala) na Nurdin Gogola (Temeke).
Osuri
Kosuli (Simiyu), Peter Amas (Arusha), Ramadhan Abdulrahman Ramadhan (Mjini
Magharibi), Renatus Mayunga (Kinondoni), Samwel Moja (Lindi), Seif Bakari
(Katavi), Shaweji Nawanda (Mtwara), Sheha Khamis Rashid (Kaskazini Unguja), Tigana
Lukinjo (Njombe), Yusuf Ramadhan Hamis (Kusini Unguja), Zahoro Mohamed (Tanga) na
Zakaria Mgambwa (Rukwa).
Waamuzi
vijana watakaoshiriki kozi hiyo chini ya Mkufunzi wa FIFA, Felix Tangawarima wa
Zimbabwe ni 33. Kwa upande wa ukocha Mkufunzi ni Ulric Mathiott kutoka
Shelisheli.
No comments:
Post a Comment