Timu
za Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro zinazojiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom (VPL)
zitacheza Jumamosi (Agosti 23 mwaka huu) mechi ya majaribio ya mfumo wa tiketi
za elektroniki.
Mechi
hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kuanzia saa 10 jioni
wakati kiingilio kitakuwa sh. 1,000.
Tiketi
za mechi hiyo zitaanza kuuzwa kesho (Agosti 20 mwaka huu) kupitia mtandao wa
M-Pesa, CRDB Simbanking na maduka 30 ya Fahari Huduma yaliyopo katika wilaya
zote za Mkoa wa Morogoro, wengi wao wakiwa Morogoro Mjini.
Washabiki
100 wa kwanza kuingia uwanjani wapata jezi za timu za Mtibwa Sugar na Polisi.
Tayari
mechi ya majaribio ya tiketi za elektroniki imeshafanyika kwenye Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo timu za Tanzania Prisons na Mbeya
City zilipambana na kutoka sare.
Mechi
nyingine za majaribio ya tiketi za elektroniki zitachezwa Agosti 30 mwaka huu.
Uwanja wa Mkwakwani jijini utakuwa na mechi kati ya Coastal Union na Mgambo
Shooting wakati katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba ni Kagera Sugar dhidi ya
mabingwa wa Mkoa wa Kagera, Eleven Stars.
Septemba
6 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa kutakuwa na mechi kati ya Simba na Mtibwa
Sugar. Mechi nyingine ni ya Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga itakayofanyika
Septemba 13 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment