Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimewaagiza wanachama wake- vyama vya mpira wa
miguu vya mikoa kuwapatia orodha ya klabu zote za mpira wa miguu zilizosajiliwa
katika mikoa yao.
Orodha
hiyo inatakiwa kujumuisha namba ya usajili wa klabu, viongozi waliopo
madarakani kwa sasa pamoja na mawasiliano yao (namba za simu na anuani za
email) na eneo yalipo makao ya klabu husika.
Kwa
utaratibu huo, vyama vya mikoa vitakusanya taarifa za klabu zinazocheza ligi ya
mikoa, lakini wakati huo vinatakiwa kuwasiliana na wanachama wake (vyama vya
wilaya) kupata taarifa za klabu zinazocheza ligi za wilaya na baadaye
kuziwasilisha TFF.
Klabu
ambazo taarifa zake zitakuwa hazijawasilishwa TFF hadi Agosti mwaka huu
hazitaruhusiwa kushiriki ligi ya msimu wa 2014/2015 katika ngazi yoyote ile.
No comments:
Post a Comment