Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza kikosi cha wachezaji 22 kwa ajili
ya mechi ya kirafiki ya kalenda ya FIFA dhidi ya Namibia (Brave Warriors)
itakayochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek, Namibia.
Wachezaji
walioitwa katika timu hiyo ni makipa Deogratius Munishi (Yanga), Ivo Mapunda
(Simba) na Mwadini Ally (Azam). Mabeki wa pembeni ni Edward Charles (JKT Ruvu),
Erasto Nyoni (Azam), Hassan Mwasapili (Mbeya City) na Michael Aidan (Ruvu
Shooting).
Mabeki
wa kati ni Aggrey Morris (Azam) na Kelvin Yondani (Yanga) wakati viungo ni Amri
Kiemba (Simba), Athuman Idd (Yanga), David Luhende (Yanga), Frank Domayo
(Yanga), Jonas Mkude (Simba) na Mwinyi Kazimoto (Markhiya Sports Club, Qatar).
Washambuliaji
ni Athanas Mdamu (Alliance Mwanza), Haruna Chanongo (Simba), Khamis Mcha
(Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Mrisho
Ngasa (Yanga), Ramadhan Singano (Simba) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe,
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaingia kambini Machi 1
mwaka huu, kwenye hoteli ya Accommondia inatarajiwa kuondoka Machi 3 mwaka huu
kwenda Windhoek.
Wachezaji
ambao timu zao zinacheza mechi za mashindano ya kimataifa na ligi wikiendi hii
wataripoti kambini mara baada ya mechi zao kumalizika.
No comments:
Post a Comment