Benchi la Tanzania Stars |
Benchi la A.S Kotoko |
TIMU ya wachezaji wa
zamani ‘Tanzania Stars’ leo imeonja kipigo cha mabao 4-3 toka kwa A.S Kotoko
FC ya Burundi katika mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Karume, Dar es
Salaam.
Tanzania Stars ilijikuta
ikionja dhahama hiyo toka kwa wageni wao katika kipindi cha kwanza na kuwafanya
kwenda mapumziko wakiwa wamefungwa mabao 4-0.
Mabao ya A.S Kotoko
yalifungwa na Nzeimana Jimmy aliyefunga mabao mawili, Said Mtoka na Amuri Salum
aliyeshindilia msumari wa mwisho.
Kipindi cha pili Tanzania
stars walibadilika na kutandaza kabumbu safi ambalo liliwavutia mashabiki
waliokuwepo uwanjani hapo na kufanikiwa kupata bao la kufuta machozi kupitia
kwa Zuberi Katwila.
Wakiendelea kutumia uzoefu
wao Tanzania stars walipata mabao mengine mawili kupitia kwa Dotto Peter kwa
njia ya penati na kufanya mchezo kumalizika kwa mabao 4-3.
Akizungumza baada ya
mchezo huo, kocha wa Tanzania Stars, Mohamed Hussein “Mmachinga’ alisema kuwa
kipigo walichokipata kinatokana na wachezaji wengi kuchelewa kufika lakini
akawasifu wapinzani wao kuwa ni wazuri na wana mbio.
“Kufungwa ni sehemu ya
mchezo ila kipigo kimetokana na wachezaji kuchelewa kufika hivyo kuanza wakiwa pungufu ila hata
hivyo wapinzani wetu ni wazuri na wana kasi sana wanapopata mpira”, alisema
Hussein.
No comments:
Post a Comment