Mshambuliaji wa Ilala, Omar Miyala akikimbia na mpira huko beki wa Kinondoni Omari Mfaume (katikati) akimkimbiza wakati wa mchezo uliochezwa Uwanja wa Karume leo |
Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa CCM, Ilala akisalimiana na wachezaji wa Ilala |
Mgeni rasmi akisalimiana na wachezaji wa Kinondoni |
Kikosi cha Kinondoni |
Kikosi cha Ilala |
TIMU ya Waamuzi wa Ilala leo waliifunga timu ya waamuzi wa Kinondoni mabao 3-0 kwenye mchezo uliochezwa
Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo ambao
ulijaa kila aina ya burudani ulishuhudia Ilala wakienda mapumziko wakiongoza
kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Kaniki Miraji akiunganisha pasi ya Emanuel
Kazimoto.
Bao la pili lilifungwa na
Said Ndege kwa njia ya penati baada ya beki wa Kinondoni kumwangusha Innocent
Mwakitamila katika eneo la goli.
Kipindi cha pili kila timu
ilifanya mabadiliko yaliyosababisha upinzani kuwa mkali kwani Kinondoni
walipata penati mara mbili lakini washambuliaji wake Hashim Abdallah na Wema
Ngotwa walipiga nje.
Wakati Kinondoni wakikosa
penati hizo Ilala nao walikosa penati moja iliyopigwa na Emanuel Kazimoto
ambaye alikuwa nyota wa mchezo huo.
Ilala walipata bao la tatu
kupitia kwa mshambuliaji mkongwe Seif Kihange aliyeunganisha krosi ya Omari
Miyala.
Akizungumza baada ya
mchezo huo Mgeni rasmi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Ilala, Asaa
Simba aliwashukuru waamuzi kwa mchezo mzuri walionesha kwani inadhihirisha kuwa
si kuchezesha tu bali pia wanajua kucheza.
“Nashukuru mmetupa
burudani ya mwaka mpya pia mmedhihirisha kuwa siyo kuchezesha wengine tu mnajua
hata kucheza na nyie mnafahamu”, alisema.
Pia walikuwepo viongozi wa
Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam, Viongozi wa chama cha soka Ilala na
viongozi wwa vyama vya waamuzi mkoa, na wilaya za mkoa wa Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment