Bao pekee lililoizamisha Ashanti lilifungwa na Joshua Oyoo dakika ya 24, akiunganisha krosi ya Ali Abondo.
Kocha Kibadeni kushoto na wasaidizi wake, Nico Kiondo na Mfaume Athumani katika mechi ya leo Uwanja wa Amaan |
Kocha mkongwe, Alhaj Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’ alibadilisha wachezaji wanne kwa mpigo mwanzoni mwa kipindi cha pili, ili kuongeza uhai katika timu yake.
Aliwatoa Anthony Matangalu, Juma Jabu, Faki Hakika na Joseph Mahundi na kuwaingiza Hussein Mkongo, Abdul Mtiro, Paul Maona na Malick Jaffar.
Pamoja na mabadiliko hayo, Ashanti iliyochukua nafasi ya Yanga SC iliyojitoa kwenye mashindano haya, haikuweza kupata bao la kusawazisha.
Kipa wa Tusker, Samuel Odhambo akiokoa hatari langoni mwake dhidi ya mshambuliaji wa Ashanti |
Mshambuliaji wa Ashanti United, Kassim Kilungo kushoto akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Tusker kulia |
Mchezaji wa Tusker akimiliki mpira mbele ya mchezaji wa Ashanti, |
Wachezaji wa Tusker kulia na wa Ashanti kushoto wakigombea mpira wa juu |
Samuel Odhiambo aliinyima mabao Ashanti leo |
Kiungo wa Ashanti, Malik Jaffar akiambaa kulia |
Kikosi cha Ashanti |
No comments:
Post a Comment