KATIBU
mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Jerome Valcke amedai kuwa
michuano ya Kombe la Dunia itakayofanyika nchini Qatar 2022 haitafanyika
mwezi Juni na Julai kama ilivyozoeleka badala yake itafanyika majira ya
baridi. Kumekuwa na mijadala mikubwa toka Qatar walipopewa uenyeji wa
kuandaa michuano hiyo Desemba mwaka 2010 kutokana na hofu ya joto kali
katika majira ya kiangazi katika ukanda huo ambalo linaweza kuwa hatari
kwa wachezaji na mashabiki watakaohudhuria. Akihojiwa na Radio France,
Valcke amesema badala ya kufanyika kipindi hicho michuano hiyo inaweza
kusogezwa mbele ya kati ya Novemba 15 na Januari 15. Valcke
aliendelea kudai kuwa kama michuano hiyo ikichezwa kati ya Novemba 15
na kumalizika Desemba muda huo hali ya hewa itakuwa nzuri tofauti na
Juni na Julai.
Modern design: The Al Wakrah Stadium is proposed to be a 40,000-seater venue
Grand designs: The proposed Al-Rayyan football stadium in Doha, to be built for the 2022 World Cup
Spectacular: The Qatar University Stadium in Doha, another one of the proposed venues
No comments:
Post a Comment