Akizungumza ofisa mtendaji wa tuzo hizo, Fredrick Luunga alisema lengo hasa ni kuthamini mchango wa makocha wazawa na wa kigeni katika kuendeleza mchezo wa soka hapa nchini.
Luunga alisema kwa miaka mingi, makocha wamekuwa wakifanya kazi hiyo katika mazingira magumu na wamekuwa hawathaminiwi vya kutosha kutokana na mchango wanaoutoa katika kupigania maendeleo ya mchezo huo.
Alisema, anaamini tuzo hiyo itakayokuwa ikitolewa kila mwaka, itasaidia kuibua ari mpya na kuwaongezea morali ya kufanya kazi makocha.
Luunga alizitaja baadhi ya tuzo hizo kuwa ni kocha bora wa mwaka, kocha wa makipa, kocha mkongwe mwenye mafanikio zaidi, kocha bora chipukizi, kocha bora wa kike, kocha bora wa kigeni, kocha wa kigeni aliyewahi kupata mafanikio makubwa alipokuwa akifundisha soka Tanzania na kocha bora mtanzania anayefundisha nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment