Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, January 8, 2014

KOCHA WA MAN UNITED AANZA VISINGIZIO, ALIA NA WAAMUZI

MENEJA wa klabu ya Manchester United, David Moyes amelalamika kuwa kikosi chake mbali na kucheza na timu pinzani lakini pia kinacheza dhidi ya waamuzi baada ya kufungwa mabao 2-1 na Sunderland katika mchezo wa mkondo wa Kombe la Ligi uliochezwa jana. Moyes ambaye yupo katika shinikizo baada ya kupoteza mechi tatu mfululizo katika mashindano yote alimnyooshea kidole mwamuzi Andre Marriner ambaye alitoa adhabu ndogo iliyowapa Sunderland bao la kwanza.  Mwamuzi huyo pia aliisaidia Sunderland kupata bao la ushindi baada ya kuwapa penati katika kipindi cha pili baada ya Adam Johnson kuangushwa katika eneo la hatari na Tom Cleverley hivyo kumpa nafasi Fabio Borini kufunga bao la penati. Akihojiwa Moyes amesema ni ngumu kuamini kuwa mwamuzi anaweza kutoa maamuzi kama yalitokea lakini hawana jinsi inabidi kusahau hayo na kuangalia michezo yao inayokuja.Moyes akiwa mazoezini na Vijana kazi wake!

Kipa  David de Gea akiwa kwenye mawazo mengi hapa!

Captain Nemanja Vidic jana baada ya kufungwa na Sunderland

Fabio alitupwa nje kwa kadi nyekundu wakati United wanacheza na Swansea hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment