LONDON, England
SIRI ya timu ya Arsenal kumnasa
kiungo wa timu ya Real Madrid, Mesut Ozil, imebainika, baada ya kuelezwa kwamba Manchester United walichelewa kutuma
ofa kwa ajili ya kumnasa nyota mwingine
wa timu hiyo, Sami Khedira.
Gazeti la El Economista lilieleza jana kuwa Real
Madrid ilikuwa na mpango wa kumuuza Khedira
badala ya Ozil, kutokana na kuwa ilikuwa ni lazima iuze mchezaji mmojawapo kwa
ajili ya kukamilisha usajili wa Gareth Bale.
Gazeti hilo lilieleza kuwa hata hivyo
ofa ya Manchester United ya pauni milioni 34 iliyokuwa ikimtaka Khedira
iliwasilishwa mjini Madrid ikiwa imechelewa, lakini ikapokelewa wakati mkataba wa Arsenal kwa Mesut Ozil ulikuwa ukijadiliwa kwa muda wa wiki kadhaa na baada ya kufikia makubaliano ya
awali baina ya klabu hizo mbili, Rais wa
Real Madrid, Florentino Perez akakubali.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa klabu
hiyo ya Old Trafford iliwasilisha ombi lake la kumtaka mchezaji huyo mwenye
umri wa miaka 26 saa moja kabla ya dirisha la usajili kufungwa, hali ambayo
ilisababisha ombi hilo lisifanikiwe.
"Kwa ujumla hatukuwa na muda wa
kulijadili jambo hilo,” alisema Ozil.
"Nilikuwa na mazungumzo na
kocha mpya, Carlo Ancelotti wiki chache
zilizopita na ilikuwa ikionekana wazi kwangu mimi nitabaki Real Madrid,” aliongeza.
Alisema kuwa wao kama wachezaji huwa
hawana ushawishi kusajiliwa kwa bei mbaya
na kwamba Real Madrid ndiyo waliokataa ofa ya Manchester United na akasema kuwa hata hivyo anafurahi kwa hilo.
No comments:
Post a Comment