SKOPJE, Macedonia
MCHEZAJI ghali duniani, Gareth Bale,
amejikuta kwenye wakati mgumu, baada ya kuvamiwa na mashabiki wawili uwanjani.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail,
mshambuliaji huyo ambaye Real Madrid imemsajili msimu huu kwa kitita cha pauni
milioni 86, alikumbana na mkasa huo wakati akiwa na timu yake ya taifa ya Wales,
akipasha misuli timu zikiwa mapumziko
katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Macedonia.
Gazeti hilo lilieleza wakati
mshambuliaji huyo wa pembeni wa timu ya Taifa ya Wales akipasha misuli na
mchezaji mwenzake wa akiba, Adam
Matthews, ghafla mashabiki wawili
wakaingia uwanjani na kuanza kumzonga nyota huyo.
Lilieleza, kutokana na hali hiyo,
ilibidi kiungo wa Celtic, Matthews kuingilia kati ili kumnusuru Bale kabla ya
maofisa usalama hawajaingilia kati kuwadhibiti vijana hao na huku Bale akionekana kupuuzia tukio hilo baada ya
kuonekana akicheka.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa inambidi
nyota huyo mwenye umri wa miaka 24
kuchukua tahadhari kutokana na umaarufu aliojiwekea tangu ajiunge na Real
Madrid, akitokea Tottenham kwa kile kinachodaiwa huenda akawa akiandamwa na
mashabiki.
Katika mchezo huo uliopigwa usiku wa
kuamkia jana mjini Skopje, Bale alikuwa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba kutokana
na hali ya wasiwasi kuhusu afya yake na hakuonekana uwanjani hata baada ya timu
yake kufungwa mabao 2-1.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
Kinda Schalke aeleza kilichomfanya azitose Arsenal, Chelsea
na Manchester City
SCHALKE, Ujerumani
NYOTA wa timu ya Schalke ya nchini
Ujerumani, Julian Draxler, amefunguka akisema kuwa aliamua kuzitosa timu kongwe
za Ligi Kuu ya England kutokana na kutamani
kukipiga kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Draxler alisema jana kuwa mwanzoni
mwa majira haya ya joto alikuwa na mawazo ya kwenda kukipiga nje ya nchi hiyo,
lakini kinda huyo mwenye umri wa miaka 19 akasema kuwa baadaye alighairi na
kuamua kuendelea kuitumikia klabu yake ya Schalke.
Hata hivyo, nyota huyo anasema kuwa
pamoja na kubadili mawazo, milango bado ipo wazi endapo ofa zitajitokeza siku
za mbele.
Kabla ya kubadili mawazo yake,
inaelezwa kuwa timu za Arsenal, Chelsea na Manchester City zilikuwa
zikipigana vikumbo zikimwania nyota huyo.
No comments:
Post a Comment