REKODI ya dunia kwenye usajili wa wachezaji imewahi
kuvunjwa mara 120 na kwa ujumla wachezaji wote waliowahi kuvunja rekodi ya
duniani thamani yao ni pauni 411,964,490 (Sh bilioni 991,202).
Dau hilo linatarajiwa kupanda na kufikiza zaidi ya
pauni milioni 500 (Sh trilioni 1.203), kama staa wa Tottenham Hotspur, Gareth
Bale ataivunja tena na kuwa mchezaji ghali zaidi duniani akitua Real Madrid.
Kwa mara ya kwanza Sheffield United walivunja rekodi
ya usajili mwaka 1913, wakafuatiwa na timu za Preston North End na Derby
County, zote mwaka 1949.
Real Madrid wamevunja rekodi ya dunia ya uhamisho
mara nne mfululizo, walianza kwa kumsajili Luis Figo, Zinedine Zidane, Kaka
na Cristiano Ronaldo.
Sasa hivi miamba hiyo ya Hispania imeweka mezani dau
la pauni milioni 85 (Sh bilioni 204.513) kwa ajili ya kunasa saini ya Gareth
Bale.
Ndiyo tunazungumzia kuhusu kuvunja rekodi ya dunia
ya uhamisho. Miaka ya nyuma haikuwa fedha nyingi sana, rekodi ya kwanza ya
duniani ilikuwa ni pauni milioni 100 (Sh bil 240,604).
Scot Willie Groves alikuwa mchezaji wa kwanza
kununuliwa kwa dau la zaidi ya pauni 100, hii ilikuwa alipohama kutoka West
Bromwich Albion kwenda Aston Villa kwa ada ya pauni 100 mwaka 1893.
Mwaka 2013 ada hiyo imekuwa mara 800,000 na rekodi
kwa sasa bado inashikiliwa na Cristiano Ronaldo, aliyetua Real Madrid kwa ada
ya pauni milioni 80 (Sh bilioni 192.483) akitokea Man United mwaka 2009.
Hadi kufikia mwaka huo rekodi ya dunia ilivunjwa
mara 41 katika nchi 12 duniani kote.
Diego Maradona amewahi kuvunja rekodi ya dunia ya
uhamisho mara mbili mfululizo – mara ya kwanza alipohama kutoka Boca Juniors
kwenda Barcelona mwaka 1982 kwa ada ya pauni milioni 3 (Sh bilioni 7.218),
miaka miwili baadaye alivunja rekodi yake alipotua Napoli kwa ada ya pauni
milioni 5 (Sh bilioni 12.03).
Luis Suarez amewahi kuvunja rekodi hiyo mara moja,
siyo Luis Suarez wa Liverpool, huyu ni Suarez wa Hispania ambaye mwaka 1961
alihama kutoka Barcelona kwenda Inter Milan kwa dau la pauni 152,000 (Sh
milioni 365.718). uhamisho wake ndio
ulikuwa wa kwanza kuvuka pauni laki moja.
Miaka 14 baadaye uhamisho wa kwanza kuvuka pauni
milioni 1 ulifanyika pale staa wa Bologna, Giuseppe Savoldi, alipohamia Napoli
kwa ada ya pauni milioni 1.2 (Sh bilioni 2.887)
England walitawala uvunjaji wa rekodi za uhamisho
kwenye nusu ya kwanza ya karne ya 20, lakini tangu mwaka 1951, Alan Shearer
ndiyo Mwingereza pekee kuvunja rekodi ya dunia ya uhamisho, pale alipohama
kutoka Blackburn Rovers kwenda Newcastle kwa ada ya pauni milioni 15 (Sh
bilioni 36.09).
Na Manchester United ndiyo timu pekee ya England
kuuza mchezaji kwa ada ya rekodi tangu mwaka 1951 pale walipomuuza Ronaldo
kwenda Real Madrid mwaka 2009.
Kabla ya mwaka 2000 Real Madrid hawakuwahi kusajili
mchezaji kwa ada ya rekodi, lakini tangu mwaka 2000, wamevunja rekodi nne
mfululizo za dunia katika usajili wa wachezaji.
Walianza kwa kumsajili Luis Figo kwa pauni milioni
37 (Sh bilioni 89.023), Zinedine Zidane pauni milioni 53 (Sh bilioni 127.52),
Kaka pauni milioni 56 (Sh bilioni 134.738) na Ronaldo na wako njiani kuvunja
rekodi hiyo kwa mara ya tano mfululizo. Ada ya usajili ya Ronaldo ni kubwa
kuliko ada za wachezaji 33 wa kwanza kuvunja rekodi ya dunia zikijumlishwa.
Orodha hii ya kuvunja rekodi ya dunia kwenye usajili
ina wachezaji kadhaa wenye majina makubwa kama kina Roberto Baggio, Ruud
Gullit, Johan Cruyff, Ronaldo de Lima na Gianluca Vialli.
Sasa hivi Bale yuko njiani kuvunja rekodi ya dunia
ya usajili kwa mara nyingine tena na Real Madrid, lakini kuna hii mizee mitatu
inayokalia dili hilo la pauni milioni 85.
Joe
Lewis
Umri:
Miaka 76
Ni
nani? Anamiliki hisa nyingi kwenye klabu ya Tottenham
Hotspur kupitia kampuni yake ya ENIC.
Utajiri
wake: Pauni bilioni 2.6 (Sh trilioni 6.255)
Utajiri
wake ameupataje: Ni mtu wa tisa kwa utajiri Uingereza na
alipata utajiri wake kwenye biashara ya kubadilisha fedha. Kwa sasa ana kampuni
ya Tavistock Group, ambayo ndani yake ipo ENIC, inayomiliki Tottenham.
Nafasi
yake kwa Bale: Hana nafasi kwa Bale, anaishi Bahamas,
mzaliwa huyo wa London hajihusishi sana na mambo ya wachezaji.
Dili
za zamani: Anaendesha klabu yake kupitia kwa Daniel Levy.
Daniel
Levy
Umri:
Miaka 51
Ni
nani? Mwenyekiti wa Spurs na Mkurugenzi Mkuu wa ENIC,
Kampuni ya michezo, vyombo vya habari na masuala ya kujiachia inayomiliki klabu
ya Tottenham. Mkurugenzi wa zamani wa Rangers.
Nafasi
yake kwa Bale: Ukweli usiopingika, Levy amekuwa na
tabia ya kuweka ngumu pale linapokuja suala la uhamisho wa wachezaji, mfano
sakata la Luka Modric ambaye aliwahi kusema kwamba alihakikishiwa kujiunga Real
Madrid, lakini alibaniwa mpaka alipogoma kucheza.
Dili
za zamani: Amewahi kufanya dili lukuki za usajili, miongoni
mwake ni Michael Carrick (pauni milioni 18 sawa na Sh bilioni 43.308) na
Dimitar Berbatov (pauni milioni 30 sawa Sh bilioni 72.181) wote walitua
Manchester United.
Jonathan
Barnett
Umri:
Miaka 63
Ni
nani? Ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Stellar Group, hii ni
kampuni ya michezo yenye ofisi zake Uingereza, Afrika na Amerika Kusini.
Kampuni hiyo inawakilisha wanamichezo 500, tangu mwaka 1994, akishirikiana na
David Manasseh. Baadhi ya wachezaji wake ni kama kina Joe Hart, Jack Butland,
Scott Sinclair, Kolo Toure na Darren Bent.
Nafasi
yake kwa Bale: Ana nafasi kubwa sana kwa Bale, ndiyo
wakala wake. Atapata asilimia tano ya 85 kama dili hilo likikubali na angependa
kumuona mchezaji wake akiwa Madrid.
Dili
za zamani: Alijipatia umaarufu sana kwa kufanikisha uhamisho
wa Ashley Cole kutoka Arsenal kwenda Chelsea, uhamisho ambao ulisababisha
afungiwe.
No comments:
Post a Comment