Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Thursday, August 1, 2013

GARETH BALE ASEMA ANATAKA KWENDA REAL MADRID

Gareth Bale ameiambia rasmi Tottenham kuwa yeye anataka kuhamia Real Madrid.

Inasemekana Bale alitua Mazoezini na pia kuendelea na matibabu yake ya maumivu ya Musuli ambako alimuambia rasmi Meneja wa Tottenham, Andre Villas-Boas, nia yake ya kuhamia Real.
Zipo taarifa kuwa Real Madrid wametoa Ofa ya Pauni Milioni 85 kumnunua Bale, ambayo ni Rekodi ya Dunia, lakini hadi sasa Tottenham hawajasema lolote kuhusu hilo licha ya kukana huko nyuma kwamba Mchezaji huyo hauzwi.
Hivi majuzi, Villas-Boas alisema anatarajia Bale atakuwa fiti kucheza Mechi yao ya Kirafiki hapo Jumamosi na Monaco ya France.
Wakati hayo yakinong’onwa, Mchezaji mmoja wa zamani wa Spurs, Jamie Redknapp, alitafakari: “Real Madrid ni Klabu kubwa Duniani, hawezi Bale kuikataa! Na naamini Tottenham ni Klabu inayouza Wachezaji wake wakubwa, historia yao inasema hivyo! Angalia nyuma Michael Carrick, Modric na Berbatov, waliuzwa! Wanauza kwa Bei muafaka kwao!”

No comments:

Post a Comment