Javier Mascherano ameomba radhi kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga mwendesha gari ya kutolea majeruhi kiwanjani katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia dhidi ya Ecuador.
Kiungo huyo wa Barcelona, ambaye aliwahi kuchezea Liverpool na West Ham, alitolewa baada ya kumpiga dereva wa gari ya kuondolea wachezaji majeruhi kiwanjani katika dakika ya 87.
Mascherano, ambaye alikuwa nahodha wa timu hiyo kwa usiku huo, baadae alisema kuwa: 'Hakuna mtu anayependa fujo nchini kwetu nilifanya makosa naona aibu kwa kufanya vile .
mwendesha gari alikuwa anakwenda kwa kasi kubwa sana ilikuwa bado kidogo nidondoke.Nilimkanya (Dereva) lakini alidharau, lakini nilichofanya hakikuwa kitendo cha kiungwana.‘Ninaelewa umuhimu wa mimi kuomba radhi na nimefedheheshwa na kwa masikitiko nimeomba radhi.’
Kwenye mtandao wa Twitter,: 'Nakiri nimefanya kitendo kibaya, hakielezeki.Baada ya kuumia , mwendesha gari alikuja kunichukua kama sheria inavyotaka japokuwa kiungo huyo, alianzisha fujo kama alivyokuwa akionekana kwenye Tv .na picha za runinga zilionyesha , Mascherano akiwa anapiga makelele kwa wahudumu wa huduma ya kwanza .
No comments:
Post a Comment