Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Wednesday, June 12, 2013

LIONEL MESSI NA BABA YAKE WAINGIA MATATANI

 



Mshambulizi wa Barcelona Lionel Messi na babake wanachunguzwa nchini Hispania kwa kuilaghai serikali ya nchi hiyo zaidi ya pauni milioni tatu nukta nne.

Mchezaji huyo kutoka Argentina na babake, Jorge wanatuhumiwa kuibia serikali ya nchi hiyo, kwa kujaza fomu zisizokuwa za ukweli za marejesho ya kodi kati ya mwaka wa 2007 na 2009.Hata hivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hajasema lolote kuhusiana na madai hayo.


Messi hulipwa Euro milioni kumi na sita kila mwaka na ndiye mchezaji anayelipwa kiasi cha juu zaidi duniani.Lakini mwendesha mashtaka Raquel Amado, aliwasilisha nyaraka za mahakama nyumbani kwake kwa mchezaji huyo katika mtaa wa kifahari wa Gava mjini Barcelona.

Jaji mjini humo ni sharti waidhinisha malalamishi dhidi ya mshukiwa yeyote kabla hajafunguliwa mashtaka.Messi na babake wanashukiwa kutumia kampuni katika mataifa ya ngambo, mjini Belize na Uruguay kuuza haki za kutumia picha ya mchezaji huyo.

Mchezaji huyo na babake wanatuhumiwa kutumia kampuni hizo zilizoko nje ya Hispania, ambako anaishi na kucheza soka ya kulipwa, kukwepa kulipa kodi inayokisiwa kuwa pauni milioni tatu na nusu.



No comments:

Post a Comment